Sunday, 20 April 2014

Dalili za mganga mchawi na ambaye ni mshirikina

Kuna waganga wengi siku hizi na wanaweka hata mabango kwenye bara bara lakini kuna waganga wachawi na washirikina na sifa zao ni hizi:

Wanapiga ramli na kujifanya kusoma nyota na  mambo ya siri wakati wao hawajui ya kwao
Wanajifanya wanagawa utajiri wakati wao si matajiri, basi kwanza wao watajirike wasaidie watu bure kama ni wakweli
Wanakuomba majina yako na ya mama yako wala si baba yako.
Wanakwambia ulete mnyama au ndege au kuku wa rangi fulani wa kuchinja na hii ni kutaka kufanya makafara kwa mashetani hasa majini ya kishetani
Wanakutakisha vitu kama nywele, nguo yenye jasho lako au la mtu unayemshugulikia
Wanaongea maneno yasiyoeleweka wakati wa tiba
Wanaita mizimu au majini eti kupandisha mizimu au kiti wanavyodai ili kuanza tiba
Wanakupa pete au hirizi la kuvaa na masharti yake
Wanakupa dawa za kuzika nyumbani au kwenye mto uzuweke uwe unazilalia
Wanakuambia uvae nguo fulani kwa siku fulani na mara kadhaa
Wanakuambia ukiamka asubuhi lazima ufanye jambo fulani kama kuzunguka nyumba yako au duka au ofisi.
Kukuamrisha kila mwezi kwenda kake kupata tiba upya au baada ya miezi kadhaa.
Kupenda pesa sana na kukwambia usipofanya hiki pesa yako itapotea utakuwa maskini au utashuka cheo
Kusema uongo kwenye tiba na kujifanya wao ndo wenye uwezo na kutoa kauli kama mimi ni hatari sana na uliza fulani na fulani nilivyofanya akawa sawa kama asingekuwa mimi asingekuwa na mafanikio hayo. Kamwe hataji uwezo wa Mungu kwenye kazi zake za tiba kabisa.
kila ukiumwa tena ukaenda kwake ukuambia ulipe gharama tena bila huruma ya kujitahidi kukutafutia dawa hili upone.
Kutajwa majina yako na unapotoka na shida yako kabla hujamwambia
Kukaa amevaa mahirizi na ring za shaba mikononi
 Kufanya kazi ya kuloga na kutibu yaani mtu akitaka kumdhuru mtu umsaidie kwa kutumia mashetani yake na akija anayeumwa atajifanya anamtibu.

Tiba zao uwaga wanaomba majini wa aina zote wawasaidie na matokea mgonjwa anapona kwa masharti na kwa kipindi fulani na baada ya miaka au kipindi kifupi anaumwa tena na anarudi kwa mganga huyu na kutoa makafara mengine ya ajabu.

Hii inasababisha tiba yao iwe ni yenye kusambaza kufuru na kufanya ushirikina wa kusambaza nguvu za giza na majini kuenea kwenye jamii na hatimaye madhara sasa yamekuwa makubwa vijijini na mjini na watu majumbani hawana amani kabisa.

Kuna dawa kama Powerful Oil, Powerful soap, Mt32(Dawa zaidi ya 32 zimesagwa na kuwa unga, zinatibu magonjwa mengi ikiwemo usioyajua ndani ya mwili bila kusahau uchawi na Safisha kwa ajili ya kupunguza mafuta, sumu na uchafu mwilini na tumboni
 
Tuwasiliane, Tutakuhudumia na Mungu atasaidia!
Email: tibaherbs@gmail.com 

 +255762053174/+255621870342

No comments:

Post a Comment