Sunday, 20 April 2014

Uchawi unavyoshambulia mwili na akili za mwanadamu

Uchawi ni tatizo siku hizi kuliko hata malaria na ukimwi kwasababu malaria na ukimwi tumeisha vitambua na kuanza kampeni za kupambana navyo kupitia vyombo vyote vya habari kama magazeti, radio, TV na Kongamano kubwa zenye kufadhiliwa na serikali husika ili kupunguza na kutokomeza magonjwa haya na mengine.

Uchawi umesambaa sana ulimwenguni na madhara yake hayachukuliwi kirasmi  na yanamhusu mwenye shida hiyo kama yeye na hakuna tiba maalum wala kipimo cha taaluma ya yule anayemsaidia kumtibu aliyelogwa kwani wenye kufanya tiba hii hawana chuo maalum kama wale wanaotibu malaria, HIV, Typhoid, Moyo. nk. Kwa hiyo aliyelogwa anafanya kujaribu kila anapoona anaweza kusaidiwa bila kuuliza elimu ya anayemtibu huo uchawi na hii inapelekea watu wengi kutapeliwa na kuwa watumwa wa waganga wasiokuwa na huruma mpaka wanawafanya wauze mali zao na kukopa ili watibiwe kwa gharama kubwa na matokeo yake haponi na wanakuwa na shida juu ya shida kutopona na kuwa maskini kiuchumi kwani wanakuwa hawazalishi mali na wanakuwa kiakili wameathirika na hawawezi kutulia na kuwa na ubunifu wa uzalisha hatima yake wanakata tamaa na kuwa tegemezi wengine wanapata stroke za kulazimisha.

Mwili wa mwanadamu unaendeshwa na mpangilio wa ajabu kiasi kwamba mifumo yote(Systems) inashirikiana kufanya mwili uwe na afya bora na hatimaye akili tulivu. Uchawi lengo kubwa ni kuvuruga mifumo ya mwili kama mfumo wa akili na mawasiliano ya mwili kiasi kwamba hata mfumo wa damu unaingiliwa na uchawi na kusababisha kiuongo cha kuratibu mifumo yote(cenral cordinating organ-ubongo) kinafanya kazi vibaya na hapo mwanadamu anaanza kujihisi kiafya hayuko salama.

Mfano uchawi kwa kusaidiwa na  mashetani katika hali zake zote kama majini, mizimu, mapepo, nk unafanya mtu asione ubaoni kama ni mwanafunzi ili asiweze kusoma na kuelewa, sasa jiulize mfumo wa kuona mashetani yaujua vizuri ndo maana yauingilia kwa njia za uchawi na mtu huyo akiwa nje anasoma vizuri hata maandishi yaliyoko mbali anayaona vizuri, mwanaume anaoa mwanamke lakini siku anapotaka kufanya tendo la ndoa shetani wa kichawi anapiga uume unaanguka na hawezi kumuingilia mke wake tena na hapa inakuwa aibu na akitoka kitandani uume unaamuka, sasa tujiulize mimi na wewe huyu shetani wa kicahwi anajuaje kuwa sehemu fulani katika mfumo wa uzazi ndo atazuia uume usiamke? Uchawi unamfanya mtu awe kichaa na tumeshuhudia ukichaa wa kulogwa na majini yanasema kuwa yametumwa yamfanye awe kichaa ili asisome au kwanini ana maisha mazuri au tulimpenda akakataa, je shetani wa uchawi au jini wa uchawi anajuaje sehemu ya ubongo ya kuathiri mpaka mtu akawa kichaa. Majibu ni haya mashetani wanamafunzo ya hali ya juu kuhusu mwili mzima wa mwanadamu na mchawi yeye hajui kwasababu unakuta kabibi au kamzee kachawi hakajui hata sehemu za mwili zinavyofanya kazi ila kanatuma mauchawi ya kudhuru watu na kuwaathiri mifumo ya uzazi, kuona, moyo, nk.kwa kutumia mashetani wenye ujuzi huo na mashetani yanapata mafunzo kwenye vyuo vyao vya kishetani sisi tusivyojua na hatuwezi kuviona kwani yenyewe yanatuona na sisi hatuyaoni mashetani na hata mchawi anayefanya nayo hayaoni ila anaona ishara na dalili na ndo maana akikosea masharti na amri zake yamamdhuru yeye.
Kwa hiyo lengo kubwa na mchawi kwa kushirikania na mashetani wa aina zote  ni kumuangamiza mwanadamu kiafya, kimali na kimaono ili awe ni mwenye kuteseka na kukata tamaa.


Tuwasiliane, Tutakuhudumia na Mungu atasaidia!
Email: tibaherbs@gmail.com 

 +255762053174/+255621870342

No comments:

Post a Comment