Saturday, 19 April 2014

UHUSIANO ULIOPO KATI YA HUSUDA NA UCHAWI

Husuda ni wivu unaoambatana na chuki ya kutaka mazuri aliyonayo mwenzako yaharibike au yeye aharibikiwe na wewe hata usipopata yale aliyonayo utafurahi kuona ameyapoteza au ameharibikiwa.
Kuna wenye wivu wa kutaka kushindana ili waweze kuiga mbinu za ufanisi uliotumika kwa wengine kupata waliyonayo mazuri au kuwa kama wao na wao kujitahidi kufanikiwa kw juhudi na bidii kubwa bila kuchukia wenzao au kuwadhuru. Hii ni sawa kuwa na wivu wa kuwa kama fulani na kumpongeza ufanisi wake na kutaka kujifunza kutoka kwake.

Husuda wa kumchukia mtu mwenye ufanisi na kheri nyingi ambazo wewe hauna ni chanzo cha kumsema vibaya kama kumsingizia kuwa mwizi, mhuni, ana roho mbaya, mchawi na watu wengi wanapokea taarifa na wanazisambaza kwa wengine baada ya muda utakuta kuwa mtaa mzima wote wanaongea kauli moja kuhusu watu fulani au mtu fulani mwenye neema kimaisha na kifamilia kumbe maskini kuna jamaa mmoja mwenye husuda alianzisha fitina hiyo siku nyingi ikasambaa taratibu na kila mtu akapokea kutoka kwenye mzunguko na kuamini kwa kusema lisemwalo na watu wengi ni kweli kumbe si lazima liwe kweli inategemea matangazo yametumika kwa nguvu na kwa mbinu gani kuwafikia watu kiasi gani. Hii fitina kama hii inazidi hata uchawi kwani madhara tumeisha yaona watu wanauawa na kuchomewa nyumba mali zao kwa fitina kama hizi. Ingawa kuna habari nyingine za kweli lakini ni muhimu kuzihakiki habari hizi na kupata ushahidi ili kutozipa nafasi fitina kuingia kwenye ukweli.
Sasa mtu akiwa na husuda ni kama mgonjwa na hata roho yake inaumia na hajui kama ana umwa husuda na hawezi kusema naumwa husuda kwa sababu hajui kuwa ni ugonjwa, baada ya hapo utamuona anakonda na kuwa na uso wenye chuki na kukunjamana bila sababu na hata anaanza kutafuta njia za kishetani kama kuanza kutafuta madawa ya ushirikina kumloga jamaa yake tena wa karibu au jirani ili ataabike na kheri alizo nazo zimtoke!

Uchawi ni kumdhuru mtu au watu na mali zao ili wasipate amani na wasifanikiwe katika kila jambo la kheri na mara nyingi mwanadamu ushirikiana na shetani kwa kufanya mkataba wa kimatambiko yaliyoko kinyume na maagizo ya Mungu mmoja wa pekee aliyeumba kila kitu, na hii ni kumchukiza Mungu kwanza na kumfurahisha shetani, ndipo shetani kwa jina lucifer na jeshi lake umpa uwezo mchawi kutumia miongoni mwa majini au mashetani yaliyoko chini ya mamlaka ya lucifer kudhuru na kuharibu watu na mali zao.

Hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kupaa kiuchawi na kuingia nyumba za watu usiku bila kufungua milango na kuwachanga watu wamelala au kuwalisha madawa ya kuwadhuru kwanza apate msaada wa mashetani ndo anaweza kufanya hivyo bila msaada huo wa mashetani hawezi kamwe kuingia ndani ya nyumba yako na kukufanya machafu hayo bila shetani kumsaidia kimkataba kama kwenda uchi makaburini, kuua mtoto wake wa kwanza kama kafara au mke, mme, mama, baba, n.k.

Mchawi kupata nguvu kubwa ya kiuchawi na kufanya makafara makubwa kama kuua anayempenda sana, kula nyama za watu, kufanya zinaa na mtoto wake, mama yake na kwa nguvu au kumkabidhi mtoto wake kwa shetani kama mke na shetani kuwa anamuingilia bila kujua ila usiku atakuwa naota anaingiliwa na wanaume au wanawake asiowajua. Mchawi nakuwa mtumwa wa shetani mpaka jamii inaanza kumuona kwa vitimbi vyake vya kujiamini kama mwenye jeshi kubwa lenye silaha za kisasa kwani akichukia tu anatoa kama mtaniona, hamnijui mimi, mtakoma, subiri siku tatu au saba au mwezi huu mtaona, na vitisho kwa kujiamini sana. Hii yote inakuwa ni kiburi na nguvu za shetani alizonazo kwani roho yake shetani anaifanya iwe ya visasi na yenye kila mara kudhuru watu na kufurahi akiona watu wanateseka na huku akijifanya ni mwenye huruma mtu akipata mkasa au akiwa mgonjwa ili jamii imuone mzuri kumbe ni chui mwneye ngozi ya kondoo.

Kwa hiyo mchawi yoyote ana husuda kubwa na mwenye husuda yoyote si lazima kuwa mchawi lakini ikikua na akawa si mwenye kuibadilisha kwenye kushindana kimaendeleo inamzuru kiafya na anakuwa mwenye uchawi wa maneno kama fitina na uongo zidi ya wenye neema kumzidi lakini husuda ikikua inazaa uchawi na kila mchawi ana husuda mbaya sana ya kuunguza roho yake na muda wote hana raha na raha yake ni kuhakikisha watu wanaomzidi neema wanashuka na kuteseka na asipofanikiwa anazidi kuteketea katika roho yake mpaka uso unachoka mapema hata kama ni kijana utafikiri mzee na mgonjwa wa muda mrefu kumbe ni husuda inamteketeza na akiloga haoni matokeo anazidi kuwa na majonzi rohoni na mwisho anaugua vidonda vya tumbo na hatimaye anadhihirika na kuhaibika kama tunaowaona kwenye vyombo vya habari mara wamekamatwa uchi kwenye nyumba za watu mara wamepotea njia mara wakutwa na vichwa vya watu, mara amempa mimba mtoto wake, mara amebaka mtoto mchanga, nk yote haya ni adhabu na majibu ya ubaya anaokuwa anafanya kwa siri kwani muda wote mwenye uchawi na husuda kwa watu wazuri hawezi kushinda.

Tuwasiliane, Tutakuhudumia na Mungu atasaidia!
Email: tibaherbs@gmail.com 

 +255762053174/+255621870342

No comments:

Post a Comment